KINANA AKAGUA UJENZI WA JENGO LA CCM MARA

0
183

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa ukumbi wa CCM mkoa wa Mara.

Kinana ameweka jiwe hilo la msingi leo Julai 26,2023 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi na utekekezaji wa ilani ya CCM.

Akizungumzia mradi huo, Katibu wa CCM wa mkoa wa Mara, Langaeli Akyo amesema hadi kukamilika kwake utagharimu shilingi Milioni 658.

Amesema asilimia 70 ya fedha hiyo tayari imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi huo Mwita Gachuma akisaidiwa na wanachama wengine tisa.

“Makamu Mwenyekiti, mkoa wa Mara una wanachama wengi wa CCM wenye uwezo, kama tutashirikiana pamoja hili jengo litaisha bila shida.” Amesema Akyo.

Amesema mradi huo wa ukumbi utakapokamilika utawezesha kufanyika Kwa vikao vya CCM na pia kuukodisha kwa ajili ya sherehe mbalimbali.