Jaji Feleshi : Kuwekwe ukomo wa muda wa kusikiliza kesi katika Mahakama Kuu

0
135

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Jaji, Dkt. Eliezer Feleshi amesema Tume ya Haki Jinai imependekaza kuwepo na muda wa kusikiliza kesi katika Mahakama Kuu ili kuhakikisha kesi zinamalizika kwa wakati na hivyo kutoa haki kwa watuhumiwa.

Jaji Feleshi amesema hatua hiyo itasaidia kuwepo kwa ukomo wa usikilizwaji wa mashtaka kwenye Mahakama Kuu na hivyo watuhumiwa kupata haki zao kwa wakati.

Ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha taarifa ya Tume ya Haki Jinai kwenye Kongamano la kujadili taarifa hiyo linalofanyika mkoani Dodoma.