Changamoto 5 zitakazosimamiwa na kampeni ya Mama Samia

0
123

Makamu wa Rais Dkt. Phillip Mpango amezitaka mamlaka husika kutatua changamoto zifuatazo kwa kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia mkoani Ruvuma, aliyoizindua mkoani hapo leo Julai 22, 2023.

  1. Kampeni ikashughulikie migogoro ya ardhi.
  2. Kampeni ikashughulikie watu walioanzisha makazi kwenye ushoroba.
  3. Kampeni ikashughulikie kesi za madai ya mirathi.
  4. Kampeni ikashughulikie migogoro ya wakulima na wafugaji. Mifugo inayoingia usiku na kusindikizwa na askari polisi wasio waadilifu.
  5. Kampeni ikashughulikie migogoro ya kazi na ajira.