Matumizi ya mifuko ya plastiki kukoma Mei 31

0
377

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amehitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020 na kusema kuwa kuanzia Juni Mosi mwaka huu itakuwa ni marufuku kutengeneza, kuingiza, kuuza na kutumia mifuko ya plastiki na matumizi ya mifuko hiyo yatakoma Mei 31 mwaka huu.