ELIMU KWA MAKONDAKTA ITOLEWE

0
155

Doris Richard ambaye ni Makamu wa Rais wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) amesema, ipo haja ya kutoa elimu kwa makondakta wa mabasi ya abiria maarufu daladala kama ilivyo kwa madereva wao.

Doris amesema hayo wakati wa majadiliano yanayoendelea hivi sasa kujadili ripoti ya Tume ya Haki Jinai katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Ameelezea kukerwa na tabia za baadhi ya makondakta hao ambazo wamekuwa wakizifanya kwa abiria wawapo safarini.

“Abiria wakisafiri wasipokuwa na amani hiyo ni changamoto kidogo, sasa mimi nilikuwa napendekeza iwepo elimu kama inavyotolewa kwa madereva na makondakta iwepo. ….Sisi watu wa chini tunapanda sana daladala lakini makondakta wa daladala kwa kweli mtu unasafiri hadi unasema hivi hii safari inaisha saa ngapii…wale sijui wanatolewa wapi wanawekwa pale, Matusi ni mengi mtu unasafiri lakini ukimaliza safari inakuwa ni changamoto,” amesema Doris