WANAOFANYA ‘HACKING’ WASILIME NA KUTENGENEZA VIATU

0
104

Mikidadi Uhuru, Mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya chuo hicho amesema, wahalifu wa makosa ya mtandao waboreshewe ujuzi ili watumie TEHAMA kwa maslahi ya Taifa.

Mikidadi ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam
alipokuwa akiwasilisha mchango wake katika mjadala wa ripoti ya Tume ya Haki Jinai.

“Wezi wengi wanapokamatwa inaonekana kazi wanazopewa ni zile ngumu ngumu tu lakini wapo vijana wanaokamatwa kwa sababu wamefanya ‘Hacking’ yani wamefanya uhalifu wa mitandao na ukiangalia kiukweli wale watu ni ‘genius’ [werevu] kwenye suala zima la IT [Tekinolojia ya mawasiliano],”

“Sasa niombe kama itawezekana kwenye magereza yetu badala ya kuweka watu wakawa tu wanalima na kutengeneza viatu waboreshewe ujuzi zaidi watumie hiyo TEHAMA kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa, mimi naamini hilo litasaidia sana,” amesema Mikidadi.