DKT. MWINYI : ELIMU NI KIPAUMBELE CHA SERIKALI

0
178

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amesema sekta ya elimu ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mujibu wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, kampasi ya Pemba.

Ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuona umuhimu wa kufungua kampasi hiyo kisiwani Pemba ikiwa ni sehemu sahihi ya kusogeza huduma za jamii katika sekta ya elimu kwa watu wa Pemba na Watanzania kwa ujumla.