Samatta asajiliwa Paok ya Ugiriki

0
241

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amejiunga na klabu ya Paok FC ya Ugiriki kutoka Fenerbahçe ya Uturuki baada ya misimu miwili ya kucheza kwa mkopo Ubelgiji.

Julai mwaka 2021 Samatta alijiunga na miamba hao wa Uturuki kwa mkataba wa miaka minne, ambapo baadaye alipelekwa kwa mkopo Ubelgiji akianzia Royal Antwerp mwaka 2021 na baadaye akarejea KRC Genk mwaka 2022.

Katika historia ya soka, Samatta alijitambulisha akiwa African Lyon mwaka 2008 kabla ya kwenda Simba 2010 ambayo ilimuuza TP Mazembe ya DR Congo mwaka 2011.

Aliwatumikia mabingwa hao wa DRC hadi mwaka 2016 alipouzwa KRC Genk ambako alidumu hadi mwaka 2020 alipouzwa Aston Villa ya England, kisha akatolewa kwa mkopo kwenda Fenerbahçe.