Tume ya marekebisho ya mfumo wa haki jinai iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan imebaini kuwa kuna udhaifu unaotendwa na Jeshi la Polisi la Tanzania na taasisi nyingine za haki jinai nchini katika kuheshimu watuhumiwa kwenye ukamataji, upelelezi, uendeshaji wa mashitaka, kuwapekua watuhumiwa wakati wanaingia magerezani na mambo mengine.
Rais Samia amesema Tanzania ikubali kuwa kuna udhaifu huo na amemuagiza Katibu Mkuu Kiongozi kuunda kamati ya kutekeleza mapendekezo mahsusi ya mageuzi ya haki jinai nchini yaliyotolewa na tume ya Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande.