Tume ya Kuboresha Mfumo na Taasisi za Haki Jinai nchini
imesema baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi nchini wamekuwa wakiwakamata watuhumiwa kabla ya kukamilisha upelelezi na wengine wakiwawekea watuhumiwa masharti magumu ya dhamana ya polisi.
Pia imesema mashtaka kwa ajili ya watuhumiwa yamekuwa yakichelewa kuandikwa Ofisi ya Taifa ya Mashkata na hiyo ni kutokana na uchache wa rasilimali watu na fedha.
Akisoma taarifa rasmi ya Tume mbele ya Rais Samia Suhulu Hassan, Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande amesema, pamoja na sheria kuelekeza mtuhumiwa asishtakiwe kabla ya upelelezi kukamilika, bado kuna ukamataji kabla ya upelelezi kukamilika na mashkata kufunguliwa mahakamani.