Tanzania yapangwa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia

0
212

Tanzania imepangwa Kundi E ktika kuwania tiketi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2026.

Katika kundi hilo, Tanzania imepangwa pamoja na Eritrea Niger, Congo, Zambia, na Morocco.

Michezo ya kuwania hatua hiyo itachezwa kwa muda wa miaka miwili ambapo michezo ya kwanza itakuwa kati ya Novemba 13 na 21 na itahitimishwa Novemba 2025.

Mashindano hayo ya 23 yatahusisha timu 48 badala ya 32 kama ilivyozoeleka, hivyo Afrika pamoja na vyama vingine vya soka vitapata nchi washiriki zaidi.

Kutokana na mabadiliko haya, mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2026 yataundwa na makundi 12, kila kundi likiwa na timu nne ambapo itashuhudia idadi ya michezo ikiongezeka kutoka 64 hadi 104 na mashindano yatachukua kati ya siku 38 hadi 40