Wacheza ngoma ya Kilua wakonga nyoyo

0
144

Kwenye picha ni Abdul’Aziz Faiz Omar na Zainab Amani Salum ambao ni wachezaji wa ngoma ya Kilua waliokonga nyoyo za Wadau wa Kiswahili katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani Kitaifa huko Zanzibar.

Wanatoka katika kikundi cha Albativile Kilua kilichopo mkoa wa Mjini Magharibi.

Ngoma ya Kilua iliingia Zanzibar kabla ya Mapinduzi kutoka Umanyema ambayo pia asili yake ni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na huchezwa kwenye shughuli mbalimbali za Kitaifa.

Ili kuwa wa mwonekano kama wa Abdul’Aziz Faiz Omar na Zainab Amani Salum hapo kwenye picha unalazimika kutumia muda wa takribani saa moja katika