Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anaendelea na ziara yake nchini Malawi, Leo ametembelea Bunge la Malawi
mjini Lilongwe ambapo amepokelewa na Spika wa Bunge hilo Fiona Kalimba.
Akiwa amefuatana na Makamu wa Rais wa Malawi, Dkt. Saulos Klaus Chilima, Rais Samia amepanda mti kama kumbukumbu ya kufanya ziara katika Bunge hilo.
Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan ameweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Malawi Dkt. Kamuzu Banda lililopo katika Makumbusho ya Kamuzu, Lilongwe.