Kampeni ya Daftari la Mama kufikia wanafunzi waishio mazingira magumu

0
160

Kuzinduliwa kwa kampeni ya daftari la Mama na Baba kutasadia kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakuta wanafunzi wa elimu ya msingi wanaosoma katika shule za serikali zizilizopo vijijini.

Wakili Philomena Mwalomgo ambaye pia ni mwenyekiti wa kampeni hiyo amesema kampeni hiyo iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam inalenga kuwagusa wanafunzi wa jinsia zote wenye uhitaji Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Steve Nyerere amesema ili Taifa liweze kusonga mbele kimaendeleo suala la ushirikiano katika kuwasadia watoto wa Kitanzania wanaoishi kwenye mazingira magumu ni jambo linalohitaji kuungwa mkono na Watanzania wote pasi kujali itikadi zao za vyama, dini na wala kabila.

Aidha, ameongeza kuwa watu wenye ulemavu ni kundi ambalo limekuwa likiachwa nyuma katika nyanja mbalimbali hivyo kutengenezwa kwa daftari maalumu kutasadia kundi hilo kwa kulitoa hatua moja hadi nyingine.

Zaidi ya wanafunzi milioni moja wanatajarajiwa kufikiwa nchi mzima kupitia kampeni hiyo.