MGOMO WA DALADALA ARUSHA

0
163

Madereva wa mabasi madogo ya abiria maarufu daladala katika jiji la Arusha, Leo wamegoma kutoa huduma ya kusafirisha abiria kwa madai ya kuwepo kwa pikipiki nyingi za magurudumu matatu
(bajaji) zinazoingilia njia za daladala.

Wamedai kuwa daladala zimekuwa zikilipa mapato ya shilingi Laki sita kwa mwaka, bima na ushuru wa barabara kila siku lakini bajaji hazilipi na bado zinaingilia njia zao.