Tumbaku yaipaisha Shinyanga

0
125

Mkoa wa Shinyanga umefanikiwa kuvuka lengo la uuzaji wa zao la Tumbaku kwa msimu uliopita ambapo zaidi ya kilo Milioni 11.8 za zao hilo zimeuzwa kwa Wafanyabiasha ambapo kilo moja imeuzwa kwa dola ya Kimarekani 2.3.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme ametoa takwimu hizo wakati akitoa salamu za mkoa huo kwenye maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani ambayo kitaifa inaadhimishwa mkoani Tabora.

Mndeme amesema kwa msimu huu mauzo yanaweza kuvunja rekodi ya mwaka 2022 kwani tangu mwezi June mwaka huu mpaka sasa tayari kilo Milioni 3 za tumbaku zimeuzwa kwa wanunuzi wa zao hilo.

Ameongeza kuwa zao hilo kwa sasa limekuwa kinara kwenye mauzo ya mazao ya biashara katika mkoa huo ambapo zaidi ya shilingi Trilioni 8.8 zimeingia katika uchumi wa wakulima na wananchi wa mkoa wa Shinyanga.