Upungufu wa Dola wakwamisha ununuzi wa Tumbaku

0
148

Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Tumbaku mkoani Tabora, Hassan Wakasuvi amesema, ununuzi wa mazao ya tumbaku umesuasua kutokana na wanunuzi wengi kulalamikia upungufu wa Dola.

Wakasuvi ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tabora amesema licha ya bei nzuri ya kununulia zao hilo katika msimu huu, wanunuzi wengi wamekuwa wakilalamikia upungufu wa Dola za Kimarekani sokoni na hivyo kushindwa kununua zao hilo.

Wakasuvi ametoa kauli hiyo wakati akitoa salamu za CCM kwenye maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani ambayo yanafanyika kitaifa katika viwanja vya Nanenane mkoani Tabora.

Hivi karibuni kumeripotiwa kuwapo kwa upungufu wa Dola za Kimarekani katika mzunguko duniani na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa ufanyaji biashara hasa zinazotumia fedha hizo kwenye kuuza na kununua.