Rais Samia afanya uteuzi

0
172

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali.

Amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mbarouk Salim Mbarouk kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Jaji Mstaafu Mbarouk ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kipindi cha pili.

Balozi Omar Ramadhan Mapuri naye ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kipindi cha pili.

Pia Rais Samia amemteua Dkt. Zakia Mohamed Abubakar kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Uteuzi wa Wajumbe hao wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi unaanza Julai Mosi 2023.

Profesa Idrissa Mshoro ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) kwa kipindi cha pili.

Benjamin Magai yeye ameteuliwa kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali.

Kabla ya uteuzi huo Magai alikuwa Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Uteuzi huo umeanza Juni 25 , 2023.