Bakwata Imewaunganisha Waislam Wote Nchini

0
123

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) Alhaj Nuhu Jabir Mruma amesema kwa takribani miaka 8 ya uongozi wa Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally, BAKWATA imewaunganisha waislamu wote nchini na kuwa kitu kimoja.

Alhaj Mruma ameyasema hayo wakati akihutubia Baraza la Eid Al Adha lililofanyika kitaifa katika Msikiti wa Mohammed VI kinondoni Dar es Salaam na kuwataka pia waumini wa dini ya kiislamu kuwa kitu kimoja.

“Sio jambo zuri mbele ya Allah (S.W), Waislamu kufarakana. Kama sisi wenyewe Waislamu tunanyosheana vidole kwa misingi ya madhehebu, au kwa hila tu za kilimwengu, basi tuelewe kuwa tutakuwa masuhuli mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiama kwa kuudhoofisha Uislamu”