HEKTA ELFU 74 ZAREJESHWA KWA WANANCHI MBARALI

0
130

Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Mbeya, Syabumi Mwaipopo ameiambia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuwa Serikali imerejesha hekta 74,432 kutoka katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwenda kwa Wananchi wa Mbarali, ili waendeleze kilimo na ufugaji.

Kamishna Mwaipopo ameyasema hayo wakati akiwasilisha ripoti kwa kamati hiyo ilipotembelea shamba la Kapunga lililoko wilayani Mbarali na kufanya tathmini ya utekelezaji wa uwekaji wa mpaka unaoendelea katika wilaya za Mbarali na Chunya mkoani Mbeya.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mohamed Mchengerwa amesema, baada ya kamati hiyo kutembelea eneo hilo na kujionea hali halisi itawasilisha mapendekezo ya walichokiona bungeni ili kubadili GN.28 na kuja na GN. mpya ambayo itakuwa ni suluhu kwa mgogoro katika eneo hilo uliodumu zaidi ya miaka 18.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Timotheo Mnzava amesema, lengo la ziara yao ni kujiridhisha ili kulishauri Bunge kuona namna bora kumaliza mgogoro huo.