Chato Beverage watumia mizizi kutengeneza vinywaji

0
218

Kiwanda cha Chato Beverage kilichopo wilayani Chato mkoani mkoani Geita kimeanza kutengeneza vinywaji vikali na baridi kwa kutumia mimea mbalimbali pamoja mizizi.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Geita, Martine Shigela wilayani Chato ambapo pia ametembelea kiwanda hicho.

Shigela amewataka wawekezaji kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini kutokana na uwepo wa rasiilimali nyingi na za aina tofauti.

Amekipongeza kiwanda hicho cha
Chato Beverage
kwa kutumia mimea ya asili na mizizi ikiwa ni pamoja na Mrondo ambao unatumiwa na kiwanda hicho kutengeneza vinywaji.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa wa Geita Profesa Godius Kahyarara amewataka wawekezaji kutumia fursa zilizopo mkoani humo kuwekeza kwa kuwa ardhi ipo ya kutosha.

Meneja Masoko wa kiwanda cha Chato Beverage Thomas Chubwa amesema, wamewekeza
zaidi ya shilingi Bilioni 1.5 kiwandani hapo na wameajiri zaidi ya watu 100 kufanyakazi katika maeneo mbalimbali.