Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewataka Viongozi na Watendaji wa Serikali wilayani Chamwino mkoani Dodoma kutoruhusu mianya ya kuwepo kwa migogoro ya ardhi katika maeneo hayo kama ilivyo kwa sehemu mbalimbali za jiji la Dodoma.
Chongolo amesema hayo alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa shule ya sekondari ya Nyerere iliyopo Chamwino, ujenzi ambao umekwama kwa muda mrefu kwa kile kinachodaiwa kuwa ni changamoto ya ukosefu wa fedha za kumalizia mradi.
Amewaambia Viongozi na Watendaji hao wa wilaya ya Chamwino kuwa
kuruhusu migogoro ya matumizi ya ardhi ambayo wangeweza kuiepusha kwa kutathmini, kupima ardhi na kuyapanga maeneo hayo
ni kutowatendea haki Wananchi.