Hali ya upatikanaji maji waimarika

0
131

Hali ya upatikanaji wa maji nchini inaendelea kuimarika ambapo kwa upande wa vijijini wastani wa upatikanaji wa maji umefikia asilimia 77 mwaka 2022 ikilinganishwa na asilimia 70.1 mwaka 2020, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba ameliambia bunge jijini Dodoma.

Aidha, kwa upande wa mijini hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi imeongezeka kutoka asilimia 84 mwaka 2020 hadi asilimia 88.0 mwaka 2022.

Dkt. Nchemba alikuwa akiwasilisha taarifa ya Hali ya Uchumi kwa mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa mwaka 2023/2024.