MV. Mwanza kukuza uchumi

0
170

Rais Samia Suluhu Hassan amesema ameridhika na maendeleo ya ujenzi wa meli ya MV. Mwanza, ambayo itasaidia kukuza biashara mkoani Mwanza, mikoa jirani na nchi jirani.

Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba mizigo hadi tani 400 kwa mara moja, itasaidia kwenye usafirisaji wa mazao katika nchi za Maziwa Makuu na hivyo kukuza uchumi wa nchi hizo.

Aidha, Rais ameahidi kurudi kuizindua MV. Mwanza itakapokamilika na kuwataka Watanzania kuendelea kutunza amani na utulivu, kwani ndio chachu kwenye biashara za Kimataifa na uwekezaji.