Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza Wakulima nchini kuongeza juhudi katika kulima mazao ya chakula na biashara, ili kuitumia vema miundombinu inayojengwa kwenye maeneo mbalimbali katika kusafirisha mazao yao.
Kwa Wakulima wa mkoa wa Mwanza na mikoa jirani, Rais Samia amewataka kutumia fursa ya ujenzi wa meli ya MV. Mwanza, daraja la JPM (Kigongo-Busisi) pamoja na miundombinu mingine inayowachochea kufanya kazi kwa bidii, lengo likiwa ni kuimarisha uchumi wao na wa Taifa.
Meli hiyo ya MV. Mwanza ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amekagua maendeleo ya ujenzi wake, mbali na kubeba abiria ina uwezo wa kubeba mizigo hadi tani 400 kwa wakati mmoja.