Daraja refu zaidi Afrika Mashariki na Kati

0
151

Rais Samia Suluhu Hassan, Leo Juni 14, 2023 amekagua na kupokea taarifa na maendeleo ya ujenzi wa daraja la JPM (Kigongo-Busisi) ambalo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 75.

Litakapokamilika, daraja hilo litakuwa ndilo daraja refu zaidi Afrika Mashariki na Kati na la sita kwa urefu Barani Afrika.

Kujengwa kwa daraja hilo la JPM kutaondoa changamoto za usafiri, kwani litakuwa likitumika kwa misimu yote bila usumbufu.

Kutokana na upekee wa daraja hilo, pia litakuwa miongoni mwa vivutio vya utalii vya mkoa wa Mwanza.