Ubora daraja la JPM ni lazima

0
162

Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa suala la ubora katika ujenzi wa daraja la JPM (Kigongo – Busisi) lazima upewe kipaumbele, kwani maisha ya watu yanategemea daraja hilo na ubovu wowote unaweza kuleta maafa.

Daraja hilo linajengwa kwa fedha za Serikali na ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Februari 24, 2024.