Rais Samia: Tuenzi utamaduni, tusiendekeze usasa

0
141


Rais Samia Suluhu Hassan amewasihi viongozi wa kimila, machifu, viongozi wa kijadi na wazazi kushirikiana kulea vijana katika maadili sahihi kwa kuzingatia mila na tamaduni za Kitanzania.

“Niwaambie machifu wenzangu kwamba pamoja na majukumu makubwa ambayo tumekabidhiwa na jamii zetu…kama wasimamizi wakuu wa maadili katika jamii tuna dhima na jukumu kubwa la kuhakikisha tunajenga Taifa bora la kesho”

“Katika sensa yetu iliyofanyika mwaka jana, tumeambiwa vijana ndio kundi kubwa sana la watu waliopo Tanzania. Vijana hawa wanataka kulelewa, kuelekezwa na kuoneshwa njia. Tukiwaacha waende wanavyoenda na usasa Taifa limeharibikiwa. Walezi wa vijana hawa ni sisi”. amesema Rais Samia

Ameongeza kwa kusema kuwa “lugha, mavazi, mila, desturi zetu, ngoma kama tulivyoona hapa, vyakula, tiba ya asili na shughuli nyingine za kijadi ni sehemu ya utamaduni wetu. Hatuna budi kuvilinda na kuviendeleza.”

Rais Samia ameyasema hayo mkoani Mwanza wakati wa Tamasha la Utamaduni Bulabo mkoani Mwanza