Mchambuzi wa Soka nchini Farhan Kihamu ametolea ufafanuzi kuhusu taarifa zilizoibuka kuwa endapo Azam atakuwa Bingwa wa Kombe la Shirikisho, Simba SC haitashiriki michuano ya Klabu Bingwa badala yake itashiriki michuano ya Shirikisho.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Farhan ameandika
“Nafasi kwa klabu za Tanzania zipo nne kimataifa, mbili klabu bingwa na mbili shirikisho! Bingwa wa Ligi Kuu na nafasi ya pili wanaenda klabu Bingwa na nafasi ya tatu na nne wanaenda shirikisho, LAKINI akitokea mfano bingwa wa FA ikawa nje ya nafasi nne za juu ataenda Shirikisho na aliyeshika nafasi ya nne Ligi atakosa ushiriki kimataifa, HATA IKITOKEA Azam wamekuwa Mabingwa wa FA bado ataenda Shirikisho kwa kuwa FA Bingwa wake nafasi yake ni Shirikisho.
Inasalia kuwa Yanga na Simba watacheza klabu bingwa 2023/24, long story short.”- ameandika Kihamu