NHIF yaelekezwa kutoa huduma hadi ngazi ya zahanati

0
251

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameuelekeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutoa huduma mpaka ngazi ya zahanati kwa vituo vyote vilivyokidhi vigezo vya kupewa huduma hiyo kikiwemo kigezo cha kusajiliwa.

Dkt. Mollel ametoa maelekezo hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Husna Juma Sekiboko.

“Nawaagiza Bima ya Afya wapite nchi nzima wahakikishe vituo vyote ambavyo vimetimiza hivi vigezo, ikiwemo kigezo cha kusajiliwa viingizwe na kuanza kutoa huduma hiyo.” Ameagiza Dkt. Mollel

Amesema katika kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora katika vituo vyote vya kutolea huduma, tayari Serikali kupitia wizara ya Afya imeagiza vifaa na vifaa tiba ambavyo vitasambazwa katika vituo mbalimbali nchini.