Waziri Chana akutana na Katibu Mkuu wa CAF

0
271

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Pindi Chana amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Veron Omba jijini Algiers nchini Algeria.

Waziri Pindi amemshukuru kwa kupokea andiko (bid) la maombi ya Tanzania, Kenya na Uganda kuandaa kwa pamoja mashindano ya AFCON mwaka 2027 akimhakikishia kuwa Tanzania imejipanga kuandaa miundombinu ya kisasa yenye viwango vya kimataifa kwa lengo la kukidhi vigezo vya CAF vya kuandaa mashindano hayo.

Veron ametumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira mazuri ya kufanyika kwa shughuli za michezo.

Mazungumzo hayo pia yamehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu pamoja na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Tanzania, Wallace Karia.