ABIRIA KUPIMWA UZITO KABLA YA SAFARI

0
147

Shirika la Ndege la New Zealand liimeanzisha utaratibu mpya wa kuwapima uzito abiria wake kabla ya kupanda ndege kwa ajili ya safari za kimataifa.

Inaelezwa kuwa utaratibu huo mpya umeanzishwa kwa lengo la kufanya uchunguzi utakaobainisha uzito wa wastani wa kila abiria ili kuboresha ufanisi katika matumizi ya mafuta ya ndege siku zijazo.

Uzito huo unarekodiwa kwa usiri katika kanzidata, ambapo hautoweza kuonekana popote kwa Wafanyakazi wa ndege au abiria.