Bandari za ziwa Victoria zavuka lengo

0
190

Bandari za ziwa Victoria zimevuka lengo katika kuhudumia shehena ya mizigo ya kutoka na kwenda nchi jirani kupitia ushoroba wa kati ,na ile inayoelekea maeneo ya visiwani na mikoa ya Mara na Kagera.

Meneja wa bandari za ziwa Victoria Ferdinand Nyathi amesema, katika mwaka wa fedha wa 2022/2023, lengo la bandari za ziwa Victoria
lilikuwa ni kuhudumia takribani tani
228, 000 za mizigo ambapo mpaka sasa wamevuka lengo na kufikia tani 246, 000 za mizigo.

Nyathi amesema mizigo inayopitia bandari za ziwa Victoria ni pamoja na malighafi za viwanda, mizigo ya bidhaa za viwandani na bidhaa za kilimo.

Nao baadhi ya Wadau wa usafirishaji wanaotumia bandari za Ziwa Victoria wamesema, maboresho yanayoendelea katika bandari za ziwa Victoria yamesaidia kuchochea biashara na shughuli za kiuchumi baina ya Tanzania na nchi jirani na katika visiwa vilivyopo ndani ya Ziwa Victoria.

Bandari za ziwa Victoria ni mjumuiko wa bandari kubwa sita, bandari ndogo tisa na bandari kavu moja, ambapo Serikali imetoa takribani shilingi Bilioni 60 ili kuziwezesha bandari hizo kufanya maboresho katika maeneo mbalimbali.