Mpishi wa Arsenal atangaza kuondoka klabuni hapo

0
174

Baada ya miaka miwili ya kuitumia Arsenal FC kama mpishi, Bernice Kariuki aliyezaliwa na kukulia Nairobi nchini Kenya amethibitisha kuwa anaondoka klabuni hapo.

Chini ya uongozi wa mpishi mkuu wa Arsenal, Kariuki amekuwa akiwapikia wachezaji wa timu ya wakubwa, uongozi wa klabu hiyo pamoja na benchi la ufundi.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook amesema msimu wa 2022/2023 ulikuwa ni msimu bora kabisa kwa Arsenal, akibainisha kuwa alifurahi kufanya kazi kwa klabu hiyo.

Mpishi huyo pia aliwashukuru Wakenya kwa msaada wao, akiongeza: “Baraka zaidi katika kazi yangu ijayo, ni kama ndoto ya kifalme, nina heshima kubwa sana… Asanteni sana hasa watu wa nchi yangu.”

Kariuki alijiunga Arsenal katikati ya mwaka 2021, baada ya Mikel Arteta kuteuliwa kuwa meneja wa Arsenal, akiwa mpishi wa kikosi cha kwanza.

Wasifu wa Bernice unaorodhesha uzoefu wake kama mpishi katika hoteli za kifahari nchini Uingereza, ikiwa ni pamoja na The Lanesborough, The Dorchester, na The Waldorf Hilton huko London akiwa ni mhitimu wa Chuo cha Westminster Kingsway ambapo alisomea sanaa ya upishi.