Radi yaua wanafamilia wawili Mkuranga

0
633

Watu wawili wa familia moja wamekufa baada ya kupigwa na radiĀ 
katika kijiji cha Kimanzichana wilayani Mkuranga mkoani Pwani.


Mwenyekiti wa kitongoji cha Nungu ambapo kipo kijiji cha
Kimanzichana, – Omari Saidi amesema kuwa radi hiyo iliambatana na
mvua kubwa na upepo mkali uliosababisha pia zaidi ya nyumba Mia
Moja kuezuliwa paa.


Saidi ameongeza kuwa mvua pamoja na upepo huo mkali
umesababisha miti mingi kuanguka na kuharibu miundombinu ya aina
mbalimbali ikiwemo ile ya barabara.
Vijiji vilivyoathiriwa zaidi na mvua pamoja na upepo mkali wilayani
Mkuranga mkoani Pwani ni Kimanzichana, Vikindu na Kazole.