Yanga yavuna milioni 95 za Rais Samia

0
163

Mwanasheria wa Yanga, Patrick Simon amesema Hamasa ya Rais Samia Suluhu Hassan imeongeza mafanikio ya timu ya Yanga kwa kiwango kikubwa.

Akizungumza na wanahabari Dar es Salaam, Simon amesema hadi sasa Yanga imepata kiasi cha milioni 95 kutokana na hamasa ya Rais Samia na bado ameendelea kutoa motisha kubwa kwa timu hiyo.

Pia Rais ametoa ndege ambayo itabeba abiria 260 ikiwa ni pamoja na wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki watakaokwenda kwenye marudio ya fainali huko Algeria

“Yanga tunaishukuru sana Serikali kwa kutekeleza maelekezo ya Rais aliposema viongozi wanaohusika na michezo kushirikiana na viongozi wa Yanga kuendelea na maandalizi na hakika mazungumzo na maandalizi yanakwenda vizuri na Yanga hatuna la kudai kwa Serikali,” ameongeza Simon.

Aidha, ameomba vyombo vyote nchini kuendelea kuzungumzia na kuhamasisha habari za Yanga ili Watanzania kujua kinachoendelea juu ya maandalizi ya fainali ya mchezo huo wa Jumapili ambao unakwenda kuwa na hatua ya kihistori katika sekta ya michezo hapa nchini.