Lifti yaporomoka, yajeruhi watu kadhaa

0
167

Lifti iliyopo katika jengo la ghorofa la Millenium (Millenium Tower) Makumbusho, Dar es Salaam, imeporomoka na kujeruhi watu kadhaa waliokuwa wakiitumia.

Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji Patrick Afande amesema, chanzo cha lifti hiyo kuporomoka ni kuzidisha idadi ya watu tofauti na uwezo wake ambapo wakati tukio hilo linatokea ilibeba zaidi ya watu 10.

Lifti hiyo imeporomoka kutoka ghorofa ya 10 na kujeruhi watu 7 ambao wamepelekwa katika hospitali ya Kairuki, Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu.