Serikali yakabidhi Foker 50 kwa ATCL

0
461

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi  amemkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt  Leonard Chamriho ndege ya serikali aina ya Foker 50 ili naye aikabidhi kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ajili ya kubeba abiria wa kawaida  kama ilivyoagizwa na Rais John Magufuli.

Hafla ya kukabidhi ndege hiyo imefanyika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, ambapo ilikua katika uwanja huo kwa lengo la kupakwa  rangi.

Rais John Magufuli alizuia ndege hiyo kusafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya kupakwa rangi ambapo kazi hiyo ingegharimu zaidi ya Shilingi Milioni 160, na badala yake kazi hiyo imefanywa na mafundi wa ndani kwa gharama ya Shilingi Milioni Saba.