Tanzania kutangazwa kwenye Jukwaa la Uchumi Qatar

0
310

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi leo ameshiriki katika ufunguzi wa Jukwaa la Uchumi huko Doha, Qatar,
lenye lengo la kutangaza vivutio vya uwekezaji duniani.

Dkt. Mwinyi anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa hilo la uchumi Doha, Qatar.

Viongozi wa nchi mbalimbali duniani wamehudhuria ufunguzi huo, wakiwa na lengo la kutangaza na kuzungumzia fursa za uwekezaji na kiuchumi zilizopo katika nchi zao.

Kabla ya kushiriki uzinduzi huo, Dkt. Mwinyi alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Sheikh Tamim Bin Hamad Al Thani, ambaye ni Amir wa Taifa la Qatar pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda.