Majaji Wanawake kuendelea kuteuliwa

0
138

Rais Samia Suluhu Hassan amesema ataendelea kuteua Majaji Wanawake katika Mhimili wa Mahakama, ili kuleta usawa wa kijinsia.

Rais Samia ameyasema hayo Ikulu Chamwino, Dodoma wakati wa hafla ya kuwaapisha Majaji Wanane wa Mahakama ya Rufani na viongozi wengine aliowateua hivi karibuni.

Amesema anajivumia uwepo wa Wanawake wenye vigezo katika Mhimili huo wa Mahakama.