Wazazi wakimbia chanjo Rukwa

0
172

Mkoa wa Rukwa umeshindwa kufikia lengo la kuchanja watoto zaidi ya elfu 20, walio na umri wa chini ya miaka mitano.

Lengo hilo liliwekwa kufuatia mwingiliano wa raia uliopo mkoani Rukwa, ambapo kuna raia wengi kutoka nchi jirani,

Mratibu wa chanjo mkoani Rukwa, Ndenisia Ulomi amesema,
ulipofika wakati wa kuchanja, wazazi na walezii wengi waliondoka pamoja na watoto wao na kwenda katika nchi zao na hivyo watoto hao kushindwa kupata chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Amesema wazazi na walezi wengi walipopata taarifa kuwa Serikali inaendesha kampeni ya chanjo dhidi
ya magonjwa mbalimbali kwa watoto, waliondoka na kurudi katika nchi zao, na baada ya kampeni kuisha wakarejea.

Ulomi amesema
kufuatia hali hiyo, wizara ya Afya ya Tanzania imewasiliana na wizara ya Afya ya nchi hizo jirani ili kuona namna ya kuanzisha kampeni ya pamoja ya ujirani mwema, lengo likiwa ni kuwezesha watoto kupata chanjo.

Katika kipindi cha Juma moja la kutoa chanjo hiyo, watoto 10,130 ambao ni sawa na asilimia 48 ya watoto elfu 20 waliotakiwa kuchanjwa ndio wamefikiwa na chanjo hiyo mkoani Rukwa.