Serikali kupitia Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) inaendelea na ujenzi wa ofisi mpya pamoja na maabara katika kata ya Mkolani wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa TAEC Miguta Ngulimi amesema, dhamira ya Serikali ni kusogeza huduma karibu na Wananchi na kwamba kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia huduma za vibali vya mionzi pamoja na ukaguzi wa watumiaji wa vyanzo vya mionzi.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Peter Ngamilo amesema, uboreshaji wa ofisi unaendelea maeneo mbalimbali nchini ili kusogeza huduma karibu na Wananchi.