Wawekezaji wa Qatar wakaribishwa Zanzibar

0
259

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi
amewakaribisha Wawekezaji wa Qatar kuwekeza Zanzibar katika sekta ya utalii, uchumi wa Buluu pamoja na eneo jipya la uwekezaji ambalo ni utalii wa kumbi za mikutano.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Qatar, Muhamed Bin Ahmed Al-Kuwari pamoja na wadau kutoka sekta binafsi ya viwanda nchini Qatar.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA)
Shariff Ali Shariff amesema, kuna umuhimu wa kukutanisha mabaraza ya uwekezaji ya Zanzibar na Qatar ili kuimarisha uhusiano zaidi na kuongeza fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar.

Rais Mwinyi yupo Doha, Qatar
kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Kimataifa la Tatu la Uchumi.