Yanga: Tunalitaka Kombe la ASFC

0
328

Klabu ya Yanga imesema inalitaka Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na kwamba itaweka nguvu zote kuhakikisha inaibuka na ushindi kwenye mchezo wa nusu fainali.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema wanaiheshimu Singida BS na kwamba wanaamini mchezo wao wa kesho hautakuwa mwepesi.

“Tunamheshimu mpinzani ambaye tutacheza naye, ameonesha kiwango kizuri kwenye hii season [msimu] lakini ni kombe ambalo tutatia nguvu kesho tuhakikishe tunavuka kwenda fainali,.”amesema Kaze

Yanga inarudi kwenye uwanja wa CCM Liti mkoani Singida ikiwa ni wiki mbili zimepita tangu walipopata ushindi wa 2-0 dhidi ya Singida BS katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Aidha, Yanga ambayo imekuwa na msimu bora ikiwa na makombe matatu inayanyemelea, inajiandaa pia na michezo ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo itacheza dhidi ya USM Alger ya Nigeria Mei 28 na Juni 3 mwaka huu.