Inter Milan yafuzu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya

0
205

Inter Milan imefuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa jumla wa magoli 3-0 dhidi ya mahasimu wao AC Milan.

Kwa ushindi huo, Inter Milan sasa inasubiri mshindi kati ya Manchester City na Real Madrid, mchezo utakaochezwa leo, ambao utaamua ni timu ipi itafuzu fainali itakayofanyika Juni 10 jijini Instabul, Uturuki.

Inter imefuzu hatua hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010 aliposhinda taji hilo ambapo kocha Jose Mourinho aliiwezesha kutwaa makombe matatu kabla ya kutimkia Real Madrid.

Wakati Inter ikiwa na matumaini ya kutwaa kombe hilo kwa mara ya nne, kocha wa AC Milan amewapongeza wachezaji wake akisema walijituma na kustahili kushinda, lakini licha ya kutofanikiwa, wamejifunza mengi msimu huu.

Makamu wa Rais wa Inter Milan na nahodha wa zamani wa timu hiyo, Javier Zanetti ameweka wazi kuwa hatamani wakutane na Real Madrid kwenye fainali, kwani kombe hilo ni kama limewekwa kwa ajili yao wakiwa wameshinda mara 14.