Dkt. Rioba atembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria

0
327

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha ametembelea ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo Dkt. Benson Bana.

Katika mazungumzo yao wamejadili kuhusu ushirikiano kati TBC na VON.

Dkt. Rioba yupo nchini Nigeria kuhudhuria kikao cha Umoja wa Vyombo vya Habari Afrika (AUB).