Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 16, 2023 amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Bernard Membe yaliyofanyika katika kijiji cha Rondo, Chiponda mkoani Lindi.
Akizungumza na waombolezaji Waziri Mkuu Majaliwa amesema, Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kumuombea na kuenzi yote mazuri aliyowahi kufanya Marehemu Bernard Membe wakati wa uhai wake.
Bernard Membe aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, alifariki dunia Mei 12, 2023 katika hospitali ya Kairuki mkoani Dar es Salaam.
