Silaha haramu 13,500 zasalimishwa

0
292

Wananchi wa Serbia wamesalimisha silaha haramu 13,500 zinazojumuisha mabomu yaliyotengenezwa kiholela, bunduki, roketi, vifaru na silaha nyingine zisizoruhusiwa.

Serbia ilitangaza kuanza zoezi la kusalimisha silaha nchini humo kufuatia mauaji yaliyotokea katika mji wa Balkan ambapo watu 17 wengi wao wakiwa watoto waliuawa kwa kupigwa risasi.

Serikali ya Serbia
imetoa muda wa mwezi mmoja hadi Juni 8 mwaka huu kwa watu nchini humo kusalimisha silaha zote ambazo hazijasajiliwa, ikiwa ni sehemu ya msako wa silaha kufuatia mauaji hayo.

Rais Aleksandar Vucic wa Serbia ametembelea eneo zilipowekwa silaha hizo na kusema kuwa silaha zilizosalimishwa zitapelekwa kwenye viwanda vya silaha vya Serbia kwa ajili ya kutumiwa na Wanajeshi wa nchi hiyo.