Rais Samia ahamisha wakuu wa mikoa

0
181

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya wakuu wa mikoa ambapo Amos Makalla amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akitoka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Pili, Adam Malima ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Bi. Fatma Abubakar Mwassa amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera akitoka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Wakati huo huo, Albert Chalamila ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Taarifa kutoka Ikulu imeeleza kuwa uhamisho wa wakuu wa mikoa unaanza mara moja.