Majaliwa, Kikwete kuongoza mazishi ya Membe

0
158

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete, kesho wanatarajiwa kuwaongoza wakazi wa kijiji cha Rondo mkoani Lindi katika mazishi ya aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mwili wa Membe kupokelewa kijijini kwake Rondo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema, kesho asubuhi Waziri Mkuu Majaliwa na viongozi mbalimbali watawasili nyumbani kwa marehemu Membe kwa ajili ya taratibu za mazishi yatakayofanyika majira ya jioni.

Bernard Membe alifariki dunia Mei 12, 2023 katika hospitali ya Kairuki mkoani Dar es Salaam, alipopelekwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.